21 na kila mmoja aliyependa na ambaye moyo wake ulimsukuma alikuja na kuleta sadaka kwa Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kazi katika Hema la Kukutania, kwa ajili ya huduma yake yote na kwa ajili ya mavazi matakatifu. 22 Wote waliopenda, wanaume na wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Mwenyezi Mungu. 29 Waisraeli wote, wanaume na wanawake, waliopenda wakaleta mbele za Mwenyezi Mungu kwa hiari yao wenyewe sadaka kwa ajili ya kazi yote ya Mwenyezi Mungu aliyokuwa amewaagiza kuifanya kupitia kwa Musa.
Bezaleli na Oholiabu
(Kutoka 31:1-11)