Kuweka wakfu maskani ya Mungu
1 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: 2 "Simika maskani ya Mungu, lile Hema la Kukutania, katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza. 3 Weka Sanduku la Ushuhuda ndani yake na ulifunike kwa pazia. Ingiza meza na kupanga vitu vyake juu yake.