5 Kuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Al-Masihi Isa:
6 Yeye, ingawa alikuwa na asili ya Mungu hasa,
hakuona kule kuwa sawa na Mungu
kuwa kitu cha kushikilia,
7 bali alijifanya si kitu,
akachukua hali hasa ya mtumwa,
naye akazaliwa katika umbo la mwanadamu.