6 Kama vile "Ibrahimu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki."
7 Fahamuni basi kwamba wale walio na imani, hao ndio watoto wa Ibrahimu. 8 Andiko liliona tangu awali kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa Mataifa kwa imani, hivyo likatangulia kumtangazia Ibrahimu Injili, likisema kwamba, "Kupitia kwako mataifa yote yatabarikiwa." 9 Kwa sababu hii, wale wote wanaoamini wanabarikiwa pamoja na Ibrahimu, mtu wa imani.