Wazao wa Tera
27 Hivi ndivyo vizazi vya Tera.
Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Lutu. 28 Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa katika Uru ya Wakaldayo, nchi aliyozaliwa.
31 Tera akawachukua Abramu mwanawe, mjukuu wake Lutu mwana wa Harani, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka Uru ya Wakaldayo pamoja, wakaenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko.