5 Lakini Mwenyezi Mungu akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu walikuwa wanaujenga. 6 Mwenyezi Mungu akasema, "Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. 7 Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao."
8 Hivyo Mwenyezi Mungu akawatawanya kutoka mahali pale waende duniani kote; nao wakaacha kuujenga huo mji. 9 Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Mwenyezi Mungu akawatawanya duniani kote.