Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 12

Wito wa Abramu

1 Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Abramu, "Ondoka katika nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonesha.

2 "Nitakufanya taifa kubwa

na nitakubariki,

Nitalikuza jina lako,

nawe utakuwa baraka.

3 Nitawabariki wale wanaokubariki,

na yeyote akulaaniye nitamlaani;

na kupitia kwako mataifa yote duniani

yatabarikiwa."

Veja também