18 Siku hiyo Mwenyezi Mungu akafanya agano na Abramu, na kumwambia, "Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia Kijito cha Misri15:18 Kijito cha Misri ina maana Wadi-el-Arish kwenye mpaka wa kusini wa Yuda. hadi mto ule mkubwa, Frati: 19 yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, 20 Wahiti, Waperizi, Warefai, 21 Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi."
Publicidade