9 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia, "Niletee ndama jike, mbuzi, na kondoo dume, kila mmoja wa miaka mitatu, pamoja na hua na kinda la njiwa."
10 Abramu akamletea hivi vyote, akampasua kila mnyama vipande viwili, akavipanga kila kimoja kuelekea mwenzake, lakini hata hivyo ndege hakuwapasua vipande viwili.
17 Jua lilipokuwa limezama na giza limeingia, tanuru la moshi na mwali wa moto unaowaka vikatokea na kupita kati ya vile vipande vya nyama. 18 Siku hiyo Mwenyezi Mungu akafanya agano na Abramu, na kumwambia, "Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia Kijito cha Misri15:18 Kijito cha Misri ina maana Wadi-el-Arish kwenye mpaka wa kusini wa Yuda. hadi mto ule mkubwa, Frati: