Pular para o conteúdo
Publicidade

Gênesis 16

Hajiri na Ishmaeli

1 Basi Sarai, mkewe Abramu, alikuwa hajamzalia watoto. Lakini alikuwa na mjakazi Mmisri jina lake Hajiri. 2 Hivyo Sarai akamwambia Abramu, "Mwenyezi Mungu amenizuilia kupata watoto. Basi nenda ukutane kimwili na mjakazi wangu; huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake."

Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema. 3 Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mjakazi wake Mmisri aliyeitwa Hajiri, na kumpa mumewe awe mke wake.

Veja também