Hajiri na Ishmaeli
1 Basi Sarai, mkewe Abramu, alikuwa hajamzalia watoto. Lakini alikuwa na mjakazi Mmisri jina lake Hajiri. 2 Hivyo Sarai akamwambia Abramu, "Mwenyezi Mungu amenizuilia kupata watoto. Basi nenda ukutane kimwili na mjakazi wangu; huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake."
Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema. 3 Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mjakazi wake Mmisri aliyeitwa Hajiri, na kumpa mumewe awe mke wake. 4 Abramu akakutana kimwili na Hajiri, naye akapata mimba.
Hajiri alipojua kuwa ana mimba, akaanza kumdharau Sarai.
16 Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita Hajiri alipomzalia Ishmaeli.