10 Kisha Mwenyezi Mungu akasema, "Hakika nitakurudia majira kama haya mwaka ujao, na Sara mkeo atakuwa na mwana."
Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema lililokuwa nyuma ya Ibrahimu. 12 Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, "Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?"
13 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Ibrahimu, "Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’ 14 Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa Mwenyezi Mungu? Nitakurudia majira kama haya mwaka ujao, naye Sara atakuwa na mwana."