22 Kisha Bwana Mwenyezi Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwa ule ubavu alioutoa kwa mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa mwanaume.
23 Huyo mwanaume akasema,
"Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu,
na nyama ya nyama yangu,
ataitwa ‘mwanamke’,
kwa kuwa alitolewa katika mwanaume."
24 Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.