Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 24:14,19,27,58,67

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

14 Basi na iwe hivi, nitakapomwambia binti mmoja, ‘Tafadhali tua mtungi wako nipate kunywa maji’; naye akisema, ‘Kunywa, nitawanywesha na ngamia wako pia’: basi na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka. Kwa hili nitajua umemtendea bwana wangu ukarimu."

19 Baada ya kumpa yule mtumishi yale maji, akamwambia, "Nitawatekea ngamia wako maji pia hadi wote watosheke."

27 akisema, "Atukuzwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ambaye hakuondoa wema na uaminifu wake kwa bwana wangu. Mimi nami, Mwenyezi Mungu ameniongoza safarini, akanifikisha nyumbani kwa jamaa za bwana wangu."

58 Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, "Je, utaenda na mtu huyu?"

Akasema, "Nitaenda."

67 Isaka akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake. Isaka akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaka akampenda; akafarijika baada ya kifo cha mama yake.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    14 Mit 19:14;Amu 6:17-37;1 Sam 6:7basi na iwe hivi; yule msichana nitakayemwambia, Tua mtungi wako, nakuomba, ninywe; naye akasema, Unywe, nami nitawanywesha na ngamia zako pia; basi huyu na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka; na kwa hayo nitajua ya kuwa umemfadhili bwana wangu. 19 Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia wako nitawatekea, hadi watakapokwisha kunywa. 27 Kut 18:10;Rut 4:14;1 Sam 25:32;2 Sam 18:28;Lk 1:68;Mwa 32:10;Zab 98:3;Mwa 24:48;Mit 3:6Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.

    58 Wakamwita Rebeka wakamwuliza, Je! Utakwenda na mtu huyu? Akasema, Nitakwenda.

    67 Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mama yake.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    14 Basi na iwe hivi, nitakapomwambia binti mmojawapo, ‘Tafadhali tua mtungi wako nipate kunywa maji,’ naye akisema, ‘Kunywa, nitawanywesha na ngamia wako pia.’ Basi na awe ndiye uliyemchagua kwa ajili ya mtumishi wako Isaki. Kwa hili nitajua umemhurumia bwana wangu."

    19 Baada ya kumpa yule mtumishi yale maji, akamwambia, "Nitateka maji kwa ajili ya ngamia zako pia mpaka wote watosheke."

    27 akisema, "Atukuzwe Bwana, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuondoa wema na uaminifu wake kwa bwana wangu. Mimi nami, Bwana ameniongoza safarini akanifikisha nyumbani kwa jamaa za bwana wangu."

    58 Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, "Je, utakwenda na mtu huyu?"

    Akasema, "Nitakwenda."

    67 Ndipo Isaki akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake, Isaki akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaki akampenda, akafarijika baada ya kifo cha mama yake.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.