Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 26

Isaka na Abimeleki

1 Basi njaa kubwa ikatokea katika nchi hiyo, mbali na njaa iliyotokea wakati wa Ibrahimu. Isaka akaenda kwa Abimeleki mfalme wa Wafilisti huko Gerari. 2 Mwenyezi Mungu akamtokea Isaka, akamwambia, "Usiende Misri, bali ukae katika nchi nitakayokuambia. 3 Kaa katika nchi hii kwa kitambo; mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote, na nitatimiza kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako. 4 Nitafanya wazao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa nchi hizi zote, na kupitia uzao wako mataifa yote yatabarikiwa, 5 kwa sababu Ibrahimu alinitii mimi, na akatenda yote niliyomwagiza, akahifadhi amri zangu, na hukumu zangu, pamoja na sheria zangu." 6 Hivyo Isaka akaishi huko Gerari.

7 Wanaume wa mahali pale walipomuuliza habari za mke wake, akasema, "Huyu ni dada yangu," kwa sababu aliogopa kusema, "Huyu ni mke wangu." Alifikiri, "Wanaume wa huku wanaweza kuniua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa ni mzuri wa sura."

8 Isaka alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki mfalme wa Wafilisti akachungulia dirishani, akaona Isaka akimpapasa Rebeka, mke wake.

Veja também