28 Mungu na akupe umande wa mbinguni
na utajiri wa duniani:
wingi wa nafaka na divai mpya.
29 Mataifa yakutumikie,
na mataifa yakusujudie.
Uwe bwana juu ya ndugu zako,
na wana wa mama yako wakusujudie.
Walaaniwe wale wanaokulaani,
na wabarikiwe wale wanaokubariki."