20 Kisha Yakobo akaweka nadhiri, akisema, "Mungu akiwa pamoja nami na kunilinda katika safari hii, akinipa chakula nile na nguo nivae, 21 na nirudi salama nyumbani mwa baba yangu, hapo ndipo Mwenyezi Mungu atakuwa Mungu wangu. 22 Nalo jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu, na katika yote utakayonipa nitakutolea sehemu ya kumi."
Mwanzo 28:20-22
Em outras traduções
- SRUV Swahili Revised Union Version
20 Mwa 28:15;31:13;Amu 11:30;2 Sam 15:8;1 Tim 6:8Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; 21 Amu 11:31;2 Sam 15:8;19:24;Kum 26:17;2 Fal 5:17nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu. 22 Mwa 35:7;Law 27:30Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
20 Kisha Yakobo akaweka nadhiri, akisema, "Kama Mungu akiwa pamoja nami na kunilinda katika safari niendayo, akinipa chakula nile na nguo nivae 21 na nirudi salama nyumbani kwa baba yangu, hapo ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu, 22 nalo jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu na katika yote utakayonipa nitakutolea wewe sehemu ya kumi."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.