17 Akamwambia Adamu, "Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’
"Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako;
kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo
siku zote za maisha yako.
18 Itakuzalia miiba na mibaruti,
nawe utakula mimea ya shambani.