12 Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani bila utulivu."
13 Kaini akamwambia Mwenyezi Mungu, "Adhabu yangu ni zaidi ya ninavyoweza kustahimili. 14 Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga duniani bila utulivu, na yeyote anionaye ataniua."
15 Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia, "La, sivyo! Ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini, atalipizwa kisasi mara saba." Kisha Mwenyezi Mungu akamwekea Kaini alama ili yeyote angemwona asimuue. 16 Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele za Mwenyezi Mungu, akaenda kuishi katika nchi ya Nodi, mashariki mwa Edeni.