Pular para o conteúdo
Publicidade

Gênesis 47

7 Ndipo Yusufu akamleta Yakobo baba yake na kumtambulisha mbele ya Farao. Baada ya Yakobo kumbariki Farao, 8 Farao akamuuliza, "Je, una umri gani?"

9 Naye Yakobo akamwambia Farao, "Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni miaka mia moja na thelathini. Miaka yangu imekuwa michache na ya taabu, wala haikufikia miaka ya maisha ya baba zangu." 10 Yakobo akambariki Farao, kisha akaondoka mbele yake.

11 Ndipo Yusufu akawakalisha baba yake na ndugu zake katika nchi ya Misri, akawapa milki katika sehemu bora sana ya nchi, ile wilaya ya Ramesesi, kama Farao alivyoelekeza. 12 Pia Yusufu akampa baba yake, na ndugu zake, na wote wa nyumbani mwa baba yake vyakula, kulingana na hesabu ya watoto wao.

Veja também