3 "Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza,
nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu;
umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo.
4 Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena,
kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako,
kwenye kitanda changu na kukinajisi.