Publicidade

Gênesis 6

13 Kwa hiyo Mungu akamwambia Nuhu, "Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika nitaangamiza watu pamoja na dunia. 14 Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje; tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. 15 Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa mia tatu6:15 Dhiraa 300 ni sawa na mita 135., upana wake dhiraa hamsini6:15 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22:5., na kimo chake dhiraa thelathini6:15 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13:5.. 16 Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja6:16 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-