8 Ndipo Mungu akamwambia Nuhu na wanawe pamoja naye: 9 "Sasa mimi ninaweka agano langu nanyi, pamoja na uzao wenu baada yenu, 10 pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: ndege, mifugo, na wanyama pori wote, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi: kila kiumbe hai duniani. 11 Ninaweka agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika; kamwe hakutakuwa tena gharika ya kuangamiza dunia."
Publicidade