Mwenyezi Mungu amesema kupitia Mwana
1 Zamani, Mungu alisema na baba zetu kupitia kwa manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, 2 lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kupitia kwa Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia kwake aliuumba ulimwengu.