Pular para o conteúdo
Publicidade

Waebrania 10:3-10

3 Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, 4 kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

5 Kwa hiyo, Al-Masihi alipokuja duniani, alisema:

"Dhabihu na sadaka hukuzitaka,

bali mwili uliniandalia;

6 sadaka za kuteketezwa na za dhambi

hukupendezwa nazo.

7 Ndipo niliposema, ‘Mimi hapa, nimekuja,

imeandikwa kunihusu katika kitabu:

Nimekuja kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu.’ "

8 Kwanza alisema, "Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo" (ingawa sheria iliagiza zitolewe). 9 Kisha akasema, "Mimi hapa, nimekuja kuyafanya mapenzi yako." Aondoa lile agano la kwanza ili kuimarisha la pili. 10 Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu kupitia kwa sadaka ya mwili wa Isa Al-Masihi alioutoa mara moja tu.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.