Kuhani Melkizedeki
1 Kwa kuwa huyu Melkizedeki alikuwa mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. Alipokutana na Ibrahimu akirudi kutoka kuwashinda wafalme, Melkizedeki alimbariki, 2 naye Ibrahimu alimpa sehemu ya kumi ya kila kitu. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake ni "mfalme wa haki". Na pia "mfalme wa Salemu" maana yake ni "mfalme wa amani".
4 Tazama jinsi alivyokuwa mkuu: Hata Ibrahimu, baba yetu wa zamani, alimpa sehemu ya kumi ya nyara zake. 9 Mtu anaweza hata kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa hiyo sehemu ya kumi kupitia kwa Ibrahimu, 10 kwa sababu Melkizedeki alipokutana na Ibrahimu, Lawi alikuwa bado katika viuno vya baba yake wa zamani.