17 Ingawa mtini hauchanui maua
na hakuna zabibu juu ya mizabibu,
ingawaje mzeituni hauzai,
na hata mashamba hayatoi chakula,
iwapo hakuna kondoo katika banda,
wala ng’ombe katika zizi,
18 hata hivyo nitashangilia katika Mwenyezi Mungu,
nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu.