Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 1:35-40

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

35 Siku iliyofuata, Yahya alikuwa huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili. 36 Alipomwona Isa akipita, akasema, "Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!"

37 Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yahya akisema haya, wakamfuata Isa. 38 Isa akageuka, akawaona wakimfuata, akawauliza, "Mnataka nini?"

Wakamwambia, "Mwalimu, unaishi wapi?"

39 Isa akawajibu, "Njooni, nanyi mtapaona!"

Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.

40 Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yahya alisema na kumfuata Isa.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    35 Tena kesho yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. 36 Yn 1:29;Isa 53:7Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu! 37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. 38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? 39 Akawaambia, Njooni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. 40 Mt 4:18-22Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    35 Siku iliyofuata, Yohana alikuwa huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili. 36 Alipomwona Yesu akipita, akasema, "Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!"

    37 Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, wakamfuata Yesu. 38 Yesu akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, "Mnataka nini?"

    Wakamwambia, "Rabi," (maana yake Mwalimu), "Unaishi wapi?"

    39 Yesu akawajibu, "Njooni, nanyi mtapaona!"

    Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.

    40 Andrea nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yohana aliyokuwa amesema, naye ndiye alimfuata Yesu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.