41 Kitu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia, "Tumemwona Masihi" (yaani Al-Masihi). 42 Naye akamleta kwa Isa.
Isa akamwangalia na kusema, "Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa" (ambalo limetafsiriwa Petro1:42 Petro kwa Kiyunani au Kefa kwa Kiaramu; maana yake Kipande cha mwamba.).