43 Siku iliyofuata Isa aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, "Nifuate."
44 Filipo alikuwa raia wa Bethsaida, mji walikotoka Andrea na Petro. 45 Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, "Tumemwona yeye ambaye Musa aliandika habari zake katika Torati, na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani Isa Al-Nasiri, mwana wa Yusufu1:45 Yusufu hakuwa baba mzazi wa Isa, bali alikuwa baba mlezi.."