45 Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, "Tumemwona yeye ambaye Musa aliandika habari zake katika Torati, na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani Isa Al-Nasiri, mwana wa Yusufu1:45 Yusufu hakuwa baba mzazi wa Isa, bali alikuwa baba mlezi.."
46 Nathanaeli akauliza, "Nasiri! Je, kitu chochote chema chaweza kutoka Nasiri?"
Filipo akamwambia, "Njoo uone."
47 Isa alipomwona Nathanaeli anakaribia, akanena habari zake, akasema, "Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli; hana hila ndani yake."
48 Nathanaeli akamuuliza, "Umenifahamuje?"
Isa akamjibu, "Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita."
49 Nathanaeli akamwambia, "Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!"
50 Isa akamwambia, "Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu kuliko hilo." 51 Ndipo akawaambia, "Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu."