14 "Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu, nao kondoo wangu wananijua. 15 Kama vile Baba10:15 Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, ndivyo nami ninautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu; hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja.