Pular para o conteúdo
Publicidade

João 12

Isa aingia Yerusalemu kwa shangwe

12 Siku iliyofuata umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Isa angekuja Yerusalemu. 13 Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema,

"Hosana!"12:13 Kiebrania kusema Okoa; basi likawa neno la shangwe.

"Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu!"

"Amebarikiwa mfalme wa Israeli!"

14 Isa akamkuta mwana-punda, akampanda, kama ilivyoandikwa,

15 "Usiogope, ewe Binti Sayuni;

tazama, mfalme wako anakuja,

amepanda mwana-punda!"

16 Wanafunzi wake Isa mwanzoni hawakuelewa mambo haya. Lakini Isa alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye.

17 Wale waliokuwepo Isa alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu waliendelea kushuhudia. 18 Na kwa sababu walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu, umati wa watu wakaenda kumlaki. 19 Hivyo Mafarisayo12:19 Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli. walipoona hayo, wakaambiana, "Mnaona, hamwezi kufanya lolote. Angalieni, ulimwengu wote unamfuata yeye!"

Veja também