21 Yeyote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye. Naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake."
22 Ndipo Yuda (siyo Iskariote) akamwambia, "Bwana, itakuwaje kwamba utajidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?"
23 Isa akamjibu, "Mtu yeyote akinipenda atalishika neno langu na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake na kufanya makao yetu kwake. 24 Mtu yeyote asiyenipenda hayashiki maneno yangu, na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma.