Pular para o conteúdo
Publicidade

João 2

Arusi huko Kana

1 Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Isa alikuwepo. 2 Isa pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. 3 Divai ilipokwisha, mama yake Isa akamwambia, "Wameishiwa na divai."

4 Isa akamwambia, "Mama, kwa nini unanihusisha? Saa yangu haijawadia."

5 Mama yake akawaambia wale watumishi, "Fanyeni lolote atakalowaambia."

6 Basi hapo palikuwa na mitungi sita iliyotengenezwa kwa mawe; iliwekwa hapo kwa ajili ya desturi ya Kiyahudi ya kujitakasa; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu2:6 Kipipa kimoja chenye ujazo wa lita 40..

7 Isa akawaambia wale watumishi, "Ijazeni hiyo mitungi maji." Nao wakaijaza ile mitungi hadi juu.

8 Kisha akawaambia, "Sasa choteni hayo maji kidogo; mpelekeeni mkuu wa sherehe."

Hivyo wakachota, wakampelekea. 9 Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilishwa kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando, 10 akamwambia, "Watu wote hutoa divai nzuri kwanza, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa sana; lakini wewe umeiweka ile nzuri zaidi hadi sasa."

11 Huu ndio muujiza wa kwanza wa Isa; aliufanya huko Kana ya Galilaya. Hivyo Isa alidhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

Veja também