Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 20

Isa awatokea wanafunzi wake

19 Ilipokuwa jioni ya siku hiyo hiyo ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walikuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa viongozi wa Wayahudi. Naye Isa akawatokea, akasimama katikati yao, akasema, "Amani iwe nanyi!" 20 Baada ya kusema haya, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi wake wakafurahi sana walipomwona Bwana Isa.

21 Isa akawaambia tena, "Amani iwe nanyi! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma ninyi." 22 Alipokwisha kusema haya, akawavuvia, akawaambia, "Pokeeni Roho Mtakatifu wa Mungu. 23 Mkimwondolea mtu yeyote dhambi zake, zitaondolewa; na yeyote msiyemwondolea dhambi zake, hazitaondolewa."

Veja também