Pular para o conteúdo
Publicidade

Yohana 20:25,27

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

25 Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, "Tumemwona Bwana Isa."

Lakini yeye akawaambia, "Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari, na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini."

27 Kisha akamwambia Tomaso, "Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyoosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu."

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    25 Yn 19:34Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.

    27 Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    25 Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, "Tumemwona Bwana."

    Lakini yeye akawaambia, "Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini."

    27 Kisha akamwambia Tomaso, "Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyoosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.