Pular para o conteúdo
Publicidade

João 21

Isa awatokea wanafunzi saba

1 Baada ya haya Isa akawatokea tena wanafunzi wake kando ya Bahari ya Tiberia21:1 yaani Bahari ya Galilaya. Yeye alijionesha kwao hivi: 2 Simoni Petro, Tomaso (aitwaye Didimasi21:2 yaani Pacha), Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo, na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. 3 Simoni Petro akawaambia wenzake, "Mimi naenda kuvua samaki." Nao wakamwambia, "Tutaenda pamoja nawe." Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua, lakini usiku ule hawakupata chochote.

4 Mara baada ya kupambazuka, Isa akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Isa.

5 Isa akawaambia, "Wanangu, je, mna samaki wowote?"

Wakamjibu, "La."

6 Akawaambia, "Shusheni nyavu upande wa kuume wa mashua yenu nanyi mtapata samaki." Wakashusha nyavu, na tazama, wakapata samaki wengi mno hata wakashindwa kuvutia zile nyavu zilizojaa samaki ndani ya mashua.

7 Basi yule mwanafunzi aliyependwa na Isa akamwambia Petro, "Huyu ni Bwana Isa!" Simoni Petro aliposikia kwamba ni Bwana Isa, akajifunga nguo yake (kwa kuwa alikuwa ameitoa), naye akajitosa baharini. 8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa mia mbili21:8 Dhiraa 200 ni kama mita 90.. 9 Walipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate.

10 Isa akawaambia, "Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi."

11 Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu ufuoni. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na watatu (153). Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.

Veja também