Isa amponya mtu kwenye Bwawa la Bethzatha
1 Baada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Isa akapanda kwenda Yerusalemu. 2 Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa Bethzatha5:2 maana yake Nyumba ya mizeituni; mahali pengine limetajwa kama Bethesda kwa Kiaramu, yaani Nyumba ya huruma, na pengine kama Bethsaida, yaani Nyumba ya uvuvi kwa Kiebrania, ambalo lilikuwa limezungukwa na makumbi matano. 3 Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe. 4 Kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji. Yule angekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao]5:3-4 Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.. 5 Mtu mmoja aliyekuwa ameugua kwa miaka thelathini na nane alikuwa hapo. 6 Isa alipomwona akiwa amelala hapo, na akijua amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu, akamwambia, "Je, wataka kuponywa?"
7 Yule mgonjwa akamjibu, "Bwana5:7 Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita "Bwana" kwa heshima ya kawaida., mimi sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Nami ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu."
8 Isa akamwambia, "Inuka! Chukua mkeka wako na uende." 9 Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea.
Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.