24 "Amin, amin nawaambia, yeyote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini na kuingia uzimani. 25 Amin, amin nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu5:25 Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (Yohana 1:1-2), wa kiroho, bali si wa kimwili., nao watakaoisikia watakuwa hai. 26 Kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake, vivyo hivyo amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake. 27 Naye amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu.
28 "Msishangae kusikia haya, kwa maana saa inakuja ambapo wale walio makaburini wataisikia sauti yake, 29 nao watatoka makaburini. Wale waliotenda mema watafufuka wapate uzima, nao wale waliotenda maovu watafufuka ili wahukumiwe.