6 Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.
7 Filipo akamjibu, "Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili6:7 Dinari 200 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 200. hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo."
8 Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia, 9 "Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa watu hawa wote?"
10 Isa akasema, "Waketisheni watu chini." Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi (palikuwa na wanaume wapatao elfu tano). 11 Ndipo Isa akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wameketi. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka.
12 Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake, "Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee chochote." 13 Hivyo wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vya ile mikate mitano ya shayiri na samaki wale wawili wadogo vilivyobakishwa na waliokula.