4 Wakamwambia Isa, "Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. 5 Katika sheria, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, hadi wafe. Sasa wewe wasemaje?" 6 Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki.
Lakini Isa akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake. 7 Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, "Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe." 8 Akainama tena na kuandika ardhini.
9 Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Isa akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake. 10 Isa akainuka na kumwambia, "Mwanamke, wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?"
11 Yule mwanamke akajibu, "Hakuna hata mmoja, Bwana."
Isa akamwambia, "Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako. Kuanzia sasa usitende dhambi tena."]8:11 Maandiko mengine ya kale hayana sehemu ya Yohana 7:53–8:11.