Pular para o conteúdo
Publicidade

Yoshua 1

6 "Uwe hodari na shujaa, kwa sababu wewe ndiwe utawaongoza watu hawa kuirithi nchi niliyowaapia baba zao kuwapa. 7 Uwe hodari na uwe na ushujaa mwingi. Uwe na bidii kutii sheria yote aliyokupa Musa mtumishi wangu; usiiache kwa kugeuka kuelekea kuume au kushoto, ili upate kufanikiwa popote utakapoenda. 9 Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuwa pamoja nawe popote utakapoenda."

Veja também