30 Naye Yefta akaweka nadhiri mbele za Mwenyezi Mungu akisema, "Ikiwa utawatia Waamoni mikononi mwangu, 31 chochote kile kitakachotoka katika mlango wa nyumba yangu cha kwanza ili kunilaki nirudipo kwa amani katika kuwashinda Waamoni, kitakuwa ni cha Mwenyezi Mungu na nitakitoa kuwa sadaka ya kuteketezwa."