3 Baba yake na mama yake wakamjibu, "Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa watu wetu wote, hata ulazimike kwenda kujitwalia mke kutoka kwa hao Wafilisti wasiotahiriwa?"
Lakini Samsoni akamwambia baba yake, "Nipatieni huyo kwa maana ndiye alinipendeza."