Pular para o conteúdo
Publicidade

Waamuzi 14:5,6

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

5 Samsoni akateremka Timna pamoja na baba yake na mama yake. Walipofika kwenye mashamba ya mizabibu huko Timna, ghafula mwana simba akamjia akimngurumia. 6 Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya Samsoni kwa nguvu, naye akampasua yule simba kwa mikono mitupu kama ambavyo angempasua mwana-mbuzi, wala hakumwambia baba yake wala mama yake alichokifanya.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    5 Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakateremka hadi Timna, walipofika katika mashamba ya mizabibu huko Timna; mara, mwanasimba akamngurumia. 6 Amu 3:10;13:25;1 Sam 11:6Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu chochote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    5 Samsoni akateremkia Timna pamoja na baba yake na mama yake. Walipofika kwenye mashamba ya mizabibu huko Timna, ghafula mwana simba akamjia akimngurumia. 6 Roho wa Bwana akaja juu yake kwa nguvu, naye akampasua yule simba kwa mikono yake bila silaha yoyote kama vile mtu ampasuavyo mwana-mbuzi, wala hakumwambia baba yake wala mama yake aliyoyafanya.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.