Pular para o conteúdo
Publicidade

Waamuzi 16:23-27

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Kifo cha Samsoni

23 Basi viongozi wa Wafilisti wakakusanyika pamoja ili kutoa kafara kuu kwa mungu wao Dagoni, wakisherehekea na kusema, "Mungu wetu amemtia adui yetu Samsoni mikononi mwetu."

24 Watu walipomwona Samsoni wakamsifu mungu wao, wakisema:

"Sasa mungu wetu amemtia adui yetu

mikononi mwetu,

yule aliyeharibu nchi yetu

na kuwaua watu wengi miongoni mwetu."

25 Mioyo yao ilipokuwa imefurahishwa, wakapaza sauti, wakisema, "Mleteni Samsoni aje ili atutumbuize." Basi wakamleta Samsoni kutoka gerezani, naye akawatumbuiza.

Wakamsimamisha katikati ya nguzo mbili. 26 Samsoni akamwambia mtumishi aliyeushika mkono wake, "Niweke mahali ambapo ninaweza kuzigusa nguzo ambazo zinategemeza jengo ili nipate kuziegemea." 27 Basi lile jengo lilikuwa na wanaume na wanawake wengi; viongozi wote wa Wafilisti walikuwa humo, na kwenye dari walikuwepo watu wapatao elfu tatu, wanaume kwa wanawake, wakimtazama Samsoni akiwatumbuiza.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    23 Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu. 24 1 Sam 31:9;1 Nya 10:9;Zab 97:7;115:3,8;Dan 5:4,23;1 Kor 8:4;10:19,20Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu. 25 Amu 9:27;16:6-9;18:20;2 Sam 13:28;1 Fal 20:12;Est 3:15;Isa 32:13;Dan 5:2-4;Mt 14:6,7Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili. 26 Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea. 27 Kum 22:8;Yos 2:6Basi nyumba ile ilikuwa imejaa wanaume kwa wanawake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu wanaume kwa wanawake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    23 Basi viongozi wa Wafilisti wakakusanyika pamoja ili kutoa kafara kwa mungu wao Dagoni na kufanya karamu, wakisema, "Mungu wetu amemtia adui yetu Samsoni mikononi mwetu."

    24 Watu walipomwona Samsoni wakamsifu mungu wao, wakisema:

    "Sasa mungu wetu amemtia adui yetu

    mikononi mwetu,

    yule aliyeharibu nchi yetu

    na kuwaua watu wengi miongoni mwetu."

    25 Mioyo yao ilipokuwa imefurahishwa wakasema, "Mleteni Samsoni aje acheze ili tufurahi." Basi wakamleta Samsoni kutoka mle gerezani naye akacheza mbele yao.

    Wakamweka kati ya nguzo mbili. 26 Samsoni akamwambia mtumishi aliyeshika mkono wake, "Niweke mahali ambapo ninaweza kuzigusa nguzo ambazo zinategemeza jengo ili nipate kuziegemea." 27 Basi lile jengo lilikuwa na wingi wa watu waume kwa wake; viongozi wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na kwenye sakafu ya juu walikuwepo watu 3,000 waume kwa wake, waliokuwa wakimtazama Samsoni wakati anacheza.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.