29 Ndipo Samsoni akazikaribia zile nguzo mbili za katikati zilizokuwa zimelisimamisha lile jengo. Akazishika moja kwa mkono wa kuume, na nyingine kwa mkono wa kushoto. 30 Samsoni akasema, "Acha nife pamoja na Wafilisti!" Ndipo akazisukuma zile nguzo kwa nguvu zake zote, nalo jengo lile likaanguka juu ya viongozi na watu wote waliokuwamo ndani. Hivyo, akawaua watu wengi wakati wa kufa kwake kuliko siku za uhai wake.
31 Basi ndugu zake na jamaa yote ya baba yake wakateremka kwenda kumchukua. Wakampandisha na kumzika kati ya Sora na Eshtaoli, kwenye kaburi la Manoa baba yake. Samsoni alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini.