Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 1

Kuzaliwa kwa Isa kwatabiriwa

26 Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Jibraili aende Galilaya katika mji wa Nasiri, 27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yusufu1:27 Yusufu hakuwa baba mzazi wa Isa, bali alikuwa baba mlezi. wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Mariamu. 28 Naye malaika akaja kwake akamwambia: "Salamu, wewe uliyebarikiwa, Mwenyezi Mungu yu pamoja nawe!"

29 Mariamu akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni salamu hii ni ya namna gani. 30 Ndipo malaika akamwambia, "Usiogope, Mariamu; umepata kibali kwa Mungu. 31 Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume na utamwita jina Isa. 32 Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Mwenyezi Mungu atampa kiti cha utawala cha Daudi baba yake. 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho."

34 Mariamu akamuuliza huyo malaika, "Maadamu mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?"

35 Malaika akamjibu, "Roho wa Mungu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli. Kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu1:35 Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (Yohana 1:1-2), wa kiroho, bali si wa kimwili.. 36 Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake, na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. 37 Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana."

38 Mariamu akasema, "Tazama, mimi ni mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Na iwe kwangu kama ulivyosema." Kisha malaika akaondoka, akamwacha.

Veja também