Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 10:25,29,36,37

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Mfano wa Msamaria mwema

25 Wakati huo mtaalamu mmoja wa Torati alisimama ili kumjaribu Isa, akamuuliza, "Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?"

29 Lakini yule mtaalamu wa Torati, akitaka kujionesha kuwa mwenye haki, akamuuliza Isa, "Jirani yangu ni nani?"

36 "Ni yupi basi miongoni mwa hawa watatu wewe unadhani ni jirani yake yule mtu aliyeangukia mikononi mwa wanyang’anyi?"

37 Yule mtaalamu wa Torati akajibu, "Ni yule aliyemhurumia."

Ndipo Isa akamwambia, "Nenda, ukafanye vivyo hivyo."

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    25 Mt 22:35-40;Mk 12:28-34Na tazama, mwanasheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?Lk 18:18-2029 Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? 36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi? 37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Nenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    25 Wakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Yesu, akamuuliza, "Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?"

    29 Lakini yule mtaalamu wa sheria, akitaka kujionyesha kuwa mwenye haki, akamuuliza Yesu, "Jirani yangu ni nani?"

    36 "Ni yupi basi miongoni mwa hawa watatu wewe unadhani ni jirani yake yule mtu aliyeangukia mikononi mwa wanyangʼanyi?"

    37 Yule mtaalamu wa sheria akajibu, "Ni yule aliyemhurumia."

    Ndipo Yesu akamwambia, "Nenda, ukafanye vivyo hivyo."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.